Ulaji bora kiafya siyo suala la masharti magumu katika filosofia ya
lishe bora,pia siyo kuwa mwembamba sana au kujinyima vyakula
unavyopenda. Isipokuwa ni kula vyakula vitakavyokufanya ujisikie vizuri,
kukuongezea nguvu mwilini, kuweka sawa afya ya akili na kujiweka katika
hali nzuri ya afya kwa kadiri iwezekanavyo; yote yanawezekana kwa
kujifunza baadhi ya kanuni za msingi za lishe bora kwa jinsi
itakavyokuwa bora kwako.
Watu wengi hufikiri kuwa lishe bora ni kula kwa wingi na siyo suala la kuzingatia mlo kamili, lakini msingi mkuu ni kula kwa kiasi chakula bora. Kiasi ni nini? Kiasi ni kiwango gani? Tunaposema kiasi, hiyo inategemea na mtu mwenyewe na tabia aliyojijengea katika ulaji wa chakula. Lengo la ulaji wa chakula bora kwa afya bora ni kujenga tabia ya kula aina ya lishe bora ambayo utaendelea kula kwa maisha yako yote, siyo tu kwa wiki chache au miezi michache mpaka pale utakapokuwa umefikia uzito ulio sawa kwa afya. Kwa hiyo jaribu kufikiri kiasi ambacho kinakutosha ili mwili uendelee kuwa na afya njema katika uzito unaokubalika wa mwili na ulaji uwe katika msingi wa mlo kamili( balanced diet).Mbali na kuwa tunapenda vyakula vyenye ladha fulani, tunahitaji pia kuzingatia mlo kamili wenye makundi ya chakula kama wanga, protini, mafuta, fiba(zapatikana katika mboga mboga,nafaka na matunda), vitamini, madini na maji, vyote hivyo kwa ajili ya kuiweka miili na akili zetu katika hali ya afya bora.
Tusijaribu kufikiri kwamba aina fulani ya kundi la chakula halifai na kuliondoa katika mlo wetu, katika hali ya asili tutajikuta tukihitaji aina ya kundi la chakula tunachojinyima na kupelekea kuongezeka kwa tamaa juu ya kundi hilo la chakula tulichojinyima, mfano mtu anaponyimwa kutumia aina fulani ya chakula kwa sababu za kiafya hujikuta anatamani sana kula aina hiyo ya chakula ambacho amenyimwa kula. Kama unavutiwa na vyakula vyenye chumvi, sukari nyingi au vyakula vingine ambavyo vikiliwa kwa wingi vinahatarisha afya, jaribu kuanza kupunguza matumizi yake kidogo kidogo mpaka utakapofikia kiwango ambacho ni bora kwa afya . Kwa kufanya hivyo utajikuta mwili wako unakuwa na afya na wenye uzito unaotakiwa na mwonekano wa kupendeza bila kukonda.
Wakati wa kula na marafiki na familia chagua aina ya chakula cha kuanzia(starter) badala ya mlo mkuu. Gawana chakula na familia na marafiki, epuka kuchukua chakula kingi kuzidi uwezo wa kula. Ukiwa nyumbani jaribu kutumia sahani ndogo zenye kuweka chakula cha kutosheleza. Endapo utajihisi haujatosheka unapomaliza, ongeza vyakula ambavyo ni mboga mboga na umalizie mlo wako kwa matunda na maji safi ya kunywa

No comments:
Post a Comment